Tuesday, August 24, 2010

yasimwayo jamiiforums

NasDaz
JF Senior Expert Member
Join DateWed May 2009
Posts 335
Thanks : 8
Thanked 84 Times in 51 Posts
Rep Power 22


. Demu wangu na wana-chadema wa jf!!
Demu wangu ana matata!! Kuona hivyo, nikalazimika kuichimba historia yake tangu ututo wake. Kumbe bana, demu wangu ni kifungua na kitinda mimba kwa baba na mama yake! Mbaya zaidi, alizaliwa wakati ambapo wazazi wakiwa wameshakata tamaa ya kupata mtoto!

Demu wangu akalelewa kama yai! Yeye akawa ni malaika kwa baba na mama yake! Hata ndugu na majirani waliotembelea pale walilazimika kumchukulia demu wangu mithili ya malaika! Nasikia Malaika hawafanyi makosa! Hali kadhalika, demu wangu nae alikuwa “hafanyi” makosa! Chochote kilichofanywa na demu, ilikuwa lazima umsifie. Nilishangaa sana siku ya kwanza nilipoingia chumbani kwake (Wakwe zangu kwa udhungu, ni kiboko! Nilikuwa nikienda pale kwao na kukuta demu wangu yupo room kwake, basi naambiwa niende hukohuko kama nina nae! Ikumbukwe, hapa ilikuwa ni mtu na boyfriend wake tu!) Kufika room, nikakuta midoli na maua kibao(ni true stori)! Demu wangu akikasirika kidogo tu, ugomvi huo hautaisha hadi anunuliwe maua na midoli! Matokeo yake room imekuwa kama ghala la maua na midoli! Demu wangu hachelewi kukasirika hata kidogo! Kutokana na hilo, wale wanaomfahamu wanalazimika kumsifia hata pale anapofanya ujinga! Juzijuzi tu hapa, akapaka wanja na shedo akatimba gheto! Unfortunately, nikasahau kwamba demu wangu wakati wote ni lazima umsifie!Badala yake, mimi nikamkosoa kwamba amekuwa kituko kutokana na wanja aliopaka! Hadi leo, ameninunia; KISA! Eti siku hizi nimebadilika sana kv nimepata demu mwingine ndo maana nilimkashifu(sikumsifia)!
Wana-CHADEMA wa JF nao ni kama demu wangu! CHADEMA, hawakosei na ni watu wanaotakiwa kusifiwa wakati wote! Hata wanapofanya ujinga; lazima tuwasifie! Hata pale tusiogemea upande wowote tunapoona wazi kwamba Slaa hawezi kumshinda JK kwenye uchaguzi huu; tulazimike kusema kwamba Slaa atashinda kwa kishindo! Wakipita mtaani na kumsikia Kibonde wa Clouds anaisifia CCM; watakurupuka na kuleta thread humu kwamba eti Kibonde anatumwa! Aaaaaa; acheni ulimbukeni bana! Wakwe zangu wamemharibu demu wangu; wana_CHADEMA wa JF mnaiharibu CHADEMA! Hamna reasoning; mnabaki kubwabwaja na mara nyingi kama sio zote mnabwabwaja bila kutoa hoja! Hoja pekee wanazoziweza ni lugha chafu na kejeli! Demu wangu nae, yupo hivyohivyo! Kila wakati; full jazba! Halafu nina mashaka kwamba wengi wenu kama sio wote ni wahuni! Huwa hamjibu hoja, zaidi ya kutoa lugha chafu kwa yeyote anayetoa changamoto dhidi ya CHADEMA! Maskini wana-CHADEMA wengi wa JF, hawajui nini maana ya CHANGAMOTO (Challenge)! Hebu tutoleeni hoja za msingi za kwanini tuipe CHADEMA ridhaa ya kuingia Ikulu!
Mimi, naamini Dk. Slaa ni kiongozi mzuri lakini chama chake hakina ubavu wa kuongeza serikali kv hakina efficiewncy manpower na mtandao wa kutosha! Urais, ni taasisi na sio sawa na kuongoza kampuni! Na hili la kutokuwa na effeciency manpower ya kutosha tayari limeshathibitishwa na CHADEMA wenyewe! Wangekuwa na manpower ya kutosha wasingekaa na kusubiria watakaotupwa na CCM ili wawadake na kuwapa shavu! Ni wao wenyewe wanaotakiwa kujilaumu kv karibu miaka 18 sasa, bado wali-opt kujikita kwenye baadhi ya maeneo tu! Sehemu yoyote utakayoona CHADEMA ina nguvu, basi ujue kuna kiongozi wa juu wa CHADEMA anayetoka sehemu hiyo! Hii ni tofauti na CCM; ambayo kila sehemu ina nguvu hata kama sehemu hiyo haina hata mwakilishi wa juu kwenye chama! Hebu tuangalie maeneo ya kujidai ya CHADEMA:
Some areas of KILIMANJARO: Kwa muasisi Mzee Mtei (The 4ma chairman) na sasa Mbowe(MWENYEKITI)! Mbaya zaidi wengi wanaamini ndiko CHADEMA ilijikita hadi kuonekana ni cha Wachaga!
Some areas of KIGOMA: Ilikuwa ni baada ya kuingia Dr. Kaborou(the former secretary general) na sasa Mheshimiwa Zitto(Deputy Secretary)
KARATU: Kwa mheshimiwa Dr.Slaa(Secretary General)


TARIME: Kwa the late Deputy Chairman Hayati Chacha Wangwe(rip)


DAR ES SALAAM: Haina mwenyewe ingawaje wengi ni wapiga domo tu na linapofika suala la maamuzi mtashangaa weenyewe!
Sasa hapo ndio mtarajie watu wenye mawazo huru tuamini kwamba CHADEMA itashinda pamoja na hilo ombwe linaloonekana wazi?!
--------------------------------------------------------------------------
 Mchambuzi

JF Senior Expert Member


Join Date

Fri Aug 2007
LocationTanzania
Posts 350
Thanks : 0
Thanked 2 Times in 1 Post


Swali kwa waratibu wa Jamiiforums
Ndugu zangu wanajamiiforums:


Hivi ni kwanini topic ambazo zinalenga kumchambua Dr. Slaa zinafutwa wakati zile zinazomlenga Kikwete zinaachwa?
Ilitegemewa kwamba jamiiforums ingekuwa ni mfano katika suala zima la uhuru wa kutoa mawazo bila ya kujali mchangiaji anatoka chama gani ilimradi havunji kanuni zilizopo. Kwanini msiachie Dr. Slaa achambuliwe ipasavyo? jamani, huyu ni mtu ambae tunategemea akipata kura za kutosha, awe ndiye raisi wetu awamu ya Tano, kwanini tunazuiana kukosoana nyakati hizi?
Niliaga jamiiforums miaka zaidi ya miwili iliyopita kutokana na tatizo hili hili ingawa nilikuwa nanyi wakati wote kwa kusoma mada mbali mbali ndani ya hii forum yetu ya jamii. Lakini nimekuwa naguswa sana na suala la kufuta baadhi ya mada wakati zingeachwa zingejenga sana ile dhana ya jamiiforums kwamba - WE DARE TO TALK OPENLY. Naomba sana waratibu wa jamiiforums mtufafanulie suala hili.
Vinginevyo Naomba sana Tujisahihishe

No comments:

Post a Comment