Wednesday, August 25, 2010

kutoka jamiiforums

Re: Slaa ameipa ushindi CCM Na Ametumika.


Originally Posted by Rev Masanilo

Mhhh another conspiracies! I beg you to communicate with ur brain before posting rubbishes and worms in the forum!

Kipepeo

Member
Join Date:Tue Feb 2008

Posts:24

Thanks : 0:Thanked 4 Times in 3 PostsRep Power:
Jibu
Ukiona mtu anatukana bila hoja ni wa kambi ya Dr Slaa.
malaria sugu kafungiwa ndani ya jamiiforums kwa udini, huu jee?


maada: Re: Hivi kwa nini CUF haina gazeti lake?
mchangiaji
Jile79
JF Senior Expert Member
Join Date:Thu May 2009
Posts:1,187
Thanks : 20:Thanked 163 Times in 114 PostsRep Power:24
majibu ya mchangiaji    26/8/2010
al nuur na al huda ndiyo vijarida vya cuf ndiyo maana haiwezi kuhangaika kuwa na kijarida kingine maana vilivyopo ni vya kidini na cuf ni taasisi ya kidini zaidi
 
hapa malaria sugu anapomshangaa moderator wa jamiiforums. huambiwa mdini anaposema wa dk slaa hufungiwa

hawa ndio wachangiaji wa jamiiforums

Kodi za kanisa ndo utendaji wake?Dr slaa anajivunia alivyowabana wakwepa kodi wa kanisani
Je huu ndo utendaji wake
KAnisani Kuna kodi gani?
Source: Raia Mwema 25.08.2010

Hivi huyu Malartia Sugu ana aliases ngapi sasa hivi? Yaani baada ya kile kipondo cha last week?

Hebu tuorodheshe hapa:
1. JeyKey
2. Tumain
3. Antibayotiki (hii ina maana anajaribu kujitafutia dawa)
4.......???
NB: Msiwe mnafupisha Malaria Sugu kwa kutumia 'MS.' Mwandikeni kwa ID yake in full -- Malaria Sugu.

baada ya kushindwa hoja, wao huona kila mtu ms tu, lkn kwanini hiyo habari si imeandikwa na raia mwema.
ms hayumo kwenye mijadala kwa sasa katika jamiiforums kwakuwa amefungiwa. kwa hivyo sihusiki na mijadala ya jamiiforums

Tuesday, August 24, 2010

JAMIIFORUMS INAPOKUWA NDUMILAKUWILI UHURU WA MAWAZO

 wahariri wa vyombo vya habari wameandamana leo asubuhi jijini Dar es salaam,maandamano hayo yalianzia mtaa wa Lugoda na kuelekea wizara ya habari utamaduni na michezo,ambako walikabidhi barua kwa Waziri wa wizara hiyo Mh George Mkuchika,aidha madhumuni ya maandamano hayo yalikuwa ni kupinga kufungiwa kwa gazeti la mwanahalisi na serikali kwa muda wa miezi 3 na pia kuishinikiza serikali ifanye marekebisho ya sheria ya uhuru wa vyombo vya habari ya mwaka 1976


Na malaria sugu
JAMIIFORUMS INAPOKUWA NDUMILAKUWILI UHURU WA MAWAZO
Ukifungua website ya jamiiforums.com utaona maandishi “jamiiforums where we dare to talk openly” ,”The Home of Great Thinkers”
Hapa utavutiwa kuingia kwa matumaini utapata uhuru wa kutoa maoni yako hasa wengi wanaochangia humo ni wale wanaharakati wa kudai uhuru zaidi wa kuapata habari, ni wale tunasoma makala zao za kusisimua kupitia magazeti, waliokuja juu baada ya baadhi ya magazeti kufungiwa chini ya utwala wa Jk, lakini pia wamo waandishi wa habari ambao wapo mbele kukosoa utwala wa awamu ya nne kwa madai ya kukandamiza uhuru wa habari, na uzuri zaidi wapo viongozi wakuu wa chama cha Chadema katika mijadala hiyo, wanaharakati hao ukiwaambia uhuru wa habari umeengezeka tangu Jk aingie madarakani hapo utaonekana mtu wa ajabu na watakuuliza upo dunia gani?unaishi wapi? Umetumwa nani kuleta uongo huu? kama huamini jaribu kuingia jamiiforums halafu uwe mfuasi wa Jk
Lakini sasa tujiulize hao wanaodai uhuru zaidi wa habari wanaohubiri ndio yaliyomo moyoni mwao?
Hapo ndipo mjadala chanya wa makala hii. Mwandishi wa makala haya alikuwa ni mmoja wachangiaji wa siku nyingi wa jamii forums , ashawahi kufanya mjadala na dk slaa , mmoja wa mjadala wake kuhusu kwanini haonekani kutabasamu katika picha zake huku akitegemea kua rais? ni mmoja ya wachangiaji wachache waliokuwa wanajenga hoja na kutetea utawala wa rais Kikwete huku saini yake (avatar) ikisomeka” ukichukia chukia, ukilia lia lakni Jk tu 2010” kumbe ujumbe huo ulikuwa mwiba kwa wenye mawazo tofauti na wao kabla ya kufungiwa na moderator siku moja tu kabla ya kampeni kuanza .
Naweza kusema 98% ya wachangiaji wa jamiiforums ni wanachadema ikiwa kama wanachama na viongozi wakuu wa chama au hata wafuasi na hadi kufikia mtandao huo kuitwa kijiwe cha chadema na wengine kuita Media ya Chadema ya kupashana habari
Wengi ambao wanatafauti na Chadema huonekana kama ni wasaliti na hawafai kuwepo katika jamii hii, wengi ambao watajaribu kuonyesha maendeleo ya liopatikana katika awamu ya JK , kukisoa Chadema huonekana kama mtu wa dunia ya mwisho na hufai kuwemo katika mijadala , lakini pia anapokuja kutetea imani yake ya kidini inapoingizwa katika maswala ya siaasa, hapo unatakiwa uwe na moyo wa jiwe na ukiwa bado unatetea mwisho hutoa shindikizo kwa moderator anaejulikana kama Invissible akufungie, na invisible hukufungia na wachangiaji ambao wana saini ya chadema huanza kupongezana.
Shindikizo zaidi limekuja baada ya baadhi ya Vyombo vya habari kuripoti uhusiano wa mgombea urais wa chadema na upadri, hapa invisible na wachangiaji wengine waliokunywa maji ya bendera za chadema wamekuwa mbogo hawataki kabisa kuona mjadala huu kuwemo katika mtandao huo, na kama utakuwa unaundeleza majina ya ajabu utapachikwa ili usambaratike na ufungiwe na moderator kwa kisingizo cha kuvunja amani na Utulivu nchini , huku wakisahau kwamba mijadala kama hiyo ya udini ya baadhi ya vyama kama CUF na CCM ilijadiliwa kipindi cha nyuma kabla ya mwandishi wa makala hizi hajajiunga katika mjadala lakini na bado inajadilwa, ukimohoji moderator kwa njia ya faragha (invessible) utatishwa kwa kufungiwa kwa kisngizio unaharibu mijadala na unaleta udini.
Gazeti au chombo cha habari kitachoripoti habari ya udini wa chadema chombo hicho huonekana kama kimevuka mipaka ya nchi,kitanangwa na kupewa kila sifa mbaya ndani ya jamiiforums kupitia wafuasi wa chadema .akitokea mwandishi wa habari hasa wa tv akimsifia rais wake wan chi au prof lipumba kwenye luninga hapo ataona chamte makuni, ataanikwa na kuanuliwa kisa kwanini amsifie .
Viongozi wakuu wa chadema ambao wanashiriki mijadala wamekuwa kimya , huku media hiyo ikionekana mbele ya sura za watu kama media ya Chadema, huku wao wakiwa mbele kutetea uhuru wa kutoa maoni sehemu nyengine, hiyo ndio chadema inayopigania kuongoza Tanzania yenye amani na utulivu .ukihoji upi msimamo wa chadema kuhusu mahakama ya kadhi na Oic wakati vyama vyengine misimamo yao ipo wazi hapo utapachikwa jina baya pengine kuitwa alqaida ndani ya jamiiforums, ukihoji Elimu ya Dk slaa itasaidiane jamii ya kitanzania hapo utasakamwa na utaichukia jamiiforums, lakini kweli leo kama watanzania pangalitokea mgombea mwenye elimu ya “master in Isalmic law” watanzania wangaliogopa kuhoji?kwanini tuogope?
Imefika wakati viongozi wa chadema kwamba wasiamini jamiiforums ndio kipimo cha ushindi, ndio maoni ya watanzania, wajue wachangiaji ambao sio wapenzi wa chadema huona michango inayotolewa na wanachadema ukumbini ndio mawazo ya chama, kejeli zinazotolewa na wanachadema ndio mawazo ya makao makuu lakini kufungia watu huku wenyewe wachangiaji na invisible huku mwenyewe wakipigania uhuru upande wa mbili hii inaweza kuweka sura mbaya kwa chadema na kwa jamiiforus kwa ujumla ,lakini hii pia inawavunja moyo wachangiaji ambao wanamawazo mazuri na nchi yetu hii, kwani chadema kama chama kinachoongozwa na binaadamu kinahaitaji kukosolewa ili kijijiue na kijipange. Chadema imeingia kwenye uchaguzi mengi yatasemwa kupitia vyombo vya habari, vipo vitaunga mkono 100% lakini vyengine vitakuwa kinyume na wao kwa 100%, yote hayo wavivumilie kama anavyovumilia JK, hawa ndio watanzania wenye mawazo tofauti, kama chama kinatakiwa kisimame imara kujitetea kuhusu udini ndani ya chama baada ya taarifa ya upadri wa dk slaa kutolewa kwani taarifa hizi bado zinaripotiwa kwenye vyombo vya habari ambavyo vinaingia hadi vijijini tofauti na jamii forums ambayo inasomwa na watu wachache tena ni wasomi tu ,lakini pia jamiiforums inaonekana dunia nzima kwa hivyo inawezekana baadhi ya wanaojadili sio wapiga kura na wanaishi mbali na Tanzania , kama chadema haitojibu hoja hizi kwa umakini mkubwa bila ya vitisho chama kinaweza kukosa wafuasi mikoa yenye waumini tofauti na imani ya Mgombea na kunyima kabisa matarjio ya chadema kuongoza nchi na kuipa ushindi wa kishindo ccm.

Mungu amjaalie Jk ashinde kwa kishindo, 88% inatosha
Malariasugu@yahoo.com
www.jktu2010.blogspot.com

yasimwayo jamiiforums

NasDaz
JF Senior Expert Member
Join DateWed May 2009
Posts 335
Thanks : 8
Thanked 84 Times in 51 Posts
Rep Power 22


. Demu wangu na wana-chadema wa jf!!
Demu wangu ana matata!! Kuona hivyo, nikalazimika kuichimba historia yake tangu ututo wake. Kumbe bana, demu wangu ni kifungua na kitinda mimba kwa baba na mama yake! Mbaya zaidi, alizaliwa wakati ambapo wazazi wakiwa wameshakata tamaa ya kupata mtoto!

Demu wangu akalelewa kama yai! Yeye akawa ni malaika kwa baba na mama yake! Hata ndugu na majirani waliotembelea pale walilazimika kumchukulia demu wangu mithili ya malaika! Nasikia Malaika hawafanyi makosa! Hali kadhalika, demu wangu nae alikuwa “hafanyi” makosa! Chochote kilichofanywa na demu, ilikuwa lazima umsifie. Nilishangaa sana siku ya kwanza nilipoingia chumbani kwake (Wakwe zangu kwa udhungu, ni kiboko! Nilikuwa nikienda pale kwao na kukuta demu wangu yupo room kwake, basi naambiwa niende hukohuko kama nina nae! Ikumbukwe, hapa ilikuwa ni mtu na boyfriend wake tu!) Kufika room, nikakuta midoli na maua kibao(ni true stori)! Demu wangu akikasirika kidogo tu, ugomvi huo hautaisha hadi anunuliwe maua na midoli! Matokeo yake room imekuwa kama ghala la maua na midoli! Demu wangu hachelewi kukasirika hata kidogo! Kutokana na hilo, wale wanaomfahamu wanalazimika kumsifia hata pale anapofanya ujinga! Juzijuzi tu hapa, akapaka wanja na shedo akatimba gheto! Unfortunately, nikasahau kwamba demu wangu wakati wote ni lazima umsifie!Badala yake, mimi nikamkosoa kwamba amekuwa kituko kutokana na wanja aliopaka! Hadi leo, ameninunia; KISA! Eti siku hizi nimebadilika sana kv nimepata demu mwingine ndo maana nilimkashifu(sikumsifia)!
Wana-CHADEMA wa JF nao ni kama demu wangu! CHADEMA, hawakosei na ni watu wanaotakiwa kusifiwa wakati wote! Hata wanapofanya ujinga; lazima tuwasifie! Hata pale tusiogemea upande wowote tunapoona wazi kwamba Slaa hawezi kumshinda JK kwenye uchaguzi huu; tulazimike kusema kwamba Slaa atashinda kwa kishindo! Wakipita mtaani na kumsikia Kibonde wa Clouds anaisifia CCM; watakurupuka na kuleta thread humu kwamba eti Kibonde anatumwa! Aaaaaa; acheni ulimbukeni bana! Wakwe zangu wamemharibu demu wangu; wana_CHADEMA wa JF mnaiharibu CHADEMA! Hamna reasoning; mnabaki kubwabwaja na mara nyingi kama sio zote mnabwabwaja bila kutoa hoja! Hoja pekee wanazoziweza ni lugha chafu na kejeli! Demu wangu nae, yupo hivyohivyo! Kila wakati; full jazba! Halafu nina mashaka kwamba wengi wenu kama sio wote ni wahuni! Huwa hamjibu hoja, zaidi ya kutoa lugha chafu kwa yeyote anayetoa changamoto dhidi ya CHADEMA! Maskini wana-CHADEMA wengi wa JF, hawajui nini maana ya CHANGAMOTO (Challenge)! Hebu tutoleeni hoja za msingi za kwanini tuipe CHADEMA ridhaa ya kuingia Ikulu!
Mimi, naamini Dk. Slaa ni kiongozi mzuri lakini chama chake hakina ubavu wa kuongeza serikali kv hakina efficiewncy manpower na mtandao wa kutosha! Urais, ni taasisi na sio sawa na kuongoza kampuni! Na hili la kutokuwa na effeciency manpower ya kutosha tayari limeshathibitishwa na CHADEMA wenyewe! Wangekuwa na manpower ya kutosha wasingekaa na kusubiria watakaotupwa na CCM ili wawadake na kuwapa shavu! Ni wao wenyewe wanaotakiwa kujilaumu kv karibu miaka 18 sasa, bado wali-opt kujikita kwenye baadhi ya maeneo tu! Sehemu yoyote utakayoona CHADEMA ina nguvu, basi ujue kuna kiongozi wa juu wa CHADEMA anayetoka sehemu hiyo! Hii ni tofauti na CCM; ambayo kila sehemu ina nguvu hata kama sehemu hiyo haina hata mwakilishi wa juu kwenye chama! Hebu tuangalie maeneo ya kujidai ya CHADEMA:
Some areas of KILIMANJARO: Kwa muasisi Mzee Mtei (The 4ma chairman) na sasa Mbowe(MWENYEKITI)! Mbaya zaidi wengi wanaamini ndiko CHADEMA ilijikita hadi kuonekana ni cha Wachaga!
Some areas of KIGOMA: Ilikuwa ni baada ya kuingia Dr. Kaborou(the former secretary general) na sasa Mheshimiwa Zitto(Deputy Secretary)
KARATU: Kwa mheshimiwa Dr.Slaa(Secretary General)


TARIME: Kwa the late Deputy Chairman Hayati Chacha Wangwe(rip)


DAR ES SALAAM: Haina mwenyewe ingawaje wengi ni wapiga domo tu na linapofika suala la maamuzi mtashangaa weenyewe!
Sasa hapo ndio mtarajie watu wenye mawazo huru tuamini kwamba CHADEMA itashinda pamoja na hilo ombwe linaloonekana wazi?!
--------------------------------------------------------------------------
 Mchambuzi

JF Senior Expert Member


Join Date

Fri Aug 2007
LocationTanzania
Posts 350
Thanks : 0
Thanked 2 Times in 1 Post


Swali kwa waratibu wa Jamiiforums
Ndugu zangu wanajamiiforums:


Hivi ni kwanini topic ambazo zinalenga kumchambua Dr. Slaa zinafutwa wakati zile zinazomlenga Kikwete zinaachwa?
Ilitegemewa kwamba jamiiforums ingekuwa ni mfano katika suala zima la uhuru wa kutoa mawazo bila ya kujali mchangiaji anatoka chama gani ilimradi havunji kanuni zilizopo. Kwanini msiachie Dr. Slaa achambuliwe ipasavyo? jamani, huyu ni mtu ambae tunategemea akipata kura za kutosha, awe ndiye raisi wetu awamu ya Tano, kwanini tunazuiana kukosoana nyakati hizi?
Niliaga jamiiforums miaka zaidi ya miwili iliyopita kutokana na tatizo hili hili ingawa nilikuwa nanyi wakati wote kwa kusoma mada mbali mbali ndani ya hii forum yetu ya jamii. Lakini nimekuwa naguswa sana na suala la kufuta baadhi ya mada wakati zingeachwa zingejenga sana ile dhana ya jamiiforums kwamba - WE DARE TO TALK OPENLY. Naomba sana waratibu wa jamiiforums mtufafanulie suala hili.
Vinginevyo Naomba sana Tujisahihishe

SIWEZI , SI UMUDU, AU SIUTAKI URAIS?

SIWEZI , SI UMUDU, AU SIUTAKI URAIS?

shein Pemba

WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA, WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) NA WANANCHI WA MKOA WA KASKAZINI PEMBA, WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR KWA TIKETI YA CCM,DK. ALI MOHAMED SHEIN ALIPOKUWA AKIWAHUTUBIA KWENYE MKUTANO WA NDANI KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA MBUYU MKAVU WETE PEMBA.
MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR KWA TIKETI YA CCM, DK. ALI MOHAMED SHEIN AKIZUNGUMZA NA WAGOMBEA WA NAFASI ZA UBUNGE, UWAKILISHI, NA UDIWANI WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM NA WANANCHI WA MKOA WA KASKAZINI PEMBA KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA MBUYU MKAVU WETE PEMBA.
MKE WA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR KWA TIKETI YA CCM, MAMA MWANAMWEMA SHEIN AKISALIMIANA NA WAJUMBE WA JUMUIYA YA WAZAZI TANZANIA NA WANANCHI WA MKOA WA KUSINI PEMBA ALIPOWASILI KATIKA UKUMBI WA UMOJA NI NGUVU MKOANI PEMBA KWA AJILI YA KUWAHUTUBIA MKUTANO WA NDANI

Monday, August 23, 2010


Nataka kuendelea kulinda uhuru wangu wa mawazo na uhuru wa kujieleza, kwani uhuru huo ni haki yangu . Na uhuru hauna kikomo, wala hakuna wakati tunapoweza kusema uhuru niliaonao unatosha. Hapana. Kila hatua inazaa matakwa mapya ya uhuru wa binadamu.
message from malaria sugu to wanajamiiforums

Sunday, August 22, 2010

karume Jangwani


Rais wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume akitia ubani uzinduzi huo


wewe mzanzibar, unangoja nini? usiitupe kura yako, mpe jk uishi kwa amani na utulivu
Marais wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mh. Benjamin Mkapa (nyuma mwenye kapelo ya kijani) wakiondoka.
wewe mtanzania unasubiri nini? Usiitupe kura yako, Mpe Jk ufaidi matunda ya neema
Karibu Jangwani, karibu kwa Jk, Usiitupe kura yako, mpe Jk uishi kwa matumaini makubwa