Tuesday, August 24, 2010

JAMIIFORUMS INAPOKUWA NDUMILAKUWILI UHURU WA MAWAZO

 wahariri wa vyombo vya habari wameandamana leo asubuhi jijini Dar es salaam,maandamano hayo yalianzia mtaa wa Lugoda na kuelekea wizara ya habari utamaduni na michezo,ambako walikabidhi barua kwa Waziri wa wizara hiyo Mh George Mkuchika,aidha madhumuni ya maandamano hayo yalikuwa ni kupinga kufungiwa kwa gazeti la mwanahalisi na serikali kwa muda wa miezi 3 na pia kuishinikiza serikali ifanye marekebisho ya sheria ya uhuru wa vyombo vya habari ya mwaka 1976


Na malaria sugu
JAMIIFORUMS INAPOKUWA NDUMILAKUWILI UHURU WA MAWAZO
Ukifungua website ya jamiiforums.com utaona maandishi “jamiiforums where we dare to talk openly” ,”The Home of Great Thinkers”
Hapa utavutiwa kuingia kwa matumaini utapata uhuru wa kutoa maoni yako hasa wengi wanaochangia humo ni wale wanaharakati wa kudai uhuru zaidi wa kuapata habari, ni wale tunasoma makala zao za kusisimua kupitia magazeti, waliokuja juu baada ya baadhi ya magazeti kufungiwa chini ya utwala wa Jk, lakini pia wamo waandishi wa habari ambao wapo mbele kukosoa utwala wa awamu ya nne kwa madai ya kukandamiza uhuru wa habari, na uzuri zaidi wapo viongozi wakuu wa chama cha Chadema katika mijadala hiyo, wanaharakati hao ukiwaambia uhuru wa habari umeengezeka tangu Jk aingie madarakani hapo utaonekana mtu wa ajabu na watakuuliza upo dunia gani?unaishi wapi? Umetumwa nani kuleta uongo huu? kama huamini jaribu kuingia jamiiforums halafu uwe mfuasi wa Jk
Lakini sasa tujiulize hao wanaodai uhuru zaidi wa habari wanaohubiri ndio yaliyomo moyoni mwao?
Hapo ndipo mjadala chanya wa makala hii. Mwandishi wa makala haya alikuwa ni mmoja wachangiaji wa siku nyingi wa jamii forums , ashawahi kufanya mjadala na dk slaa , mmoja wa mjadala wake kuhusu kwanini haonekani kutabasamu katika picha zake huku akitegemea kua rais? ni mmoja ya wachangiaji wachache waliokuwa wanajenga hoja na kutetea utawala wa rais Kikwete huku saini yake (avatar) ikisomeka” ukichukia chukia, ukilia lia lakni Jk tu 2010” kumbe ujumbe huo ulikuwa mwiba kwa wenye mawazo tofauti na wao kabla ya kufungiwa na moderator siku moja tu kabla ya kampeni kuanza .
Naweza kusema 98% ya wachangiaji wa jamiiforums ni wanachadema ikiwa kama wanachama na viongozi wakuu wa chama au hata wafuasi na hadi kufikia mtandao huo kuitwa kijiwe cha chadema na wengine kuita Media ya Chadema ya kupashana habari
Wengi ambao wanatafauti na Chadema huonekana kama ni wasaliti na hawafai kuwepo katika jamii hii, wengi ambao watajaribu kuonyesha maendeleo ya liopatikana katika awamu ya JK , kukisoa Chadema huonekana kama mtu wa dunia ya mwisho na hufai kuwemo katika mijadala , lakini pia anapokuja kutetea imani yake ya kidini inapoingizwa katika maswala ya siaasa, hapo unatakiwa uwe na moyo wa jiwe na ukiwa bado unatetea mwisho hutoa shindikizo kwa moderator anaejulikana kama Invissible akufungie, na invisible hukufungia na wachangiaji ambao wana saini ya chadema huanza kupongezana.
Shindikizo zaidi limekuja baada ya baadhi ya Vyombo vya habari kuripoti uhusiano wa mgombea urais wa chadema na upadri, hapa invisible na wachangiaji wengine waliokunywa maji ya bendera za chadema wamekuwa mbogo hawataki kabisa kuona mjadala huu kuwemo katika mtandao huo, na kama utakuwa unaundeleza majina ya ajabu utapachikwa ili usambaratike na ufungiwe na moderator kwa kisingizo cha kuvunja amani na Utulivu nchini , huku wakisahau kwamba mijadala kama hiyo ya udini ya baadhi ya vyama kama CUF na CCM ilijadiliwa kipindi cha nyuma kabla ya mwandishi wa makala hizi hajajiunga katika mjadala lakini na bado inajadilwa, ukimohoji moderator kwa njia ya faragha (invessible) utatishwa kwa kufungiwa kwa kisngizio unaharibu mijadala na unaleta udini.
Gazeti au chombo cha habari kitachoripoti habari ya udini wa chadema chombo hicho huonekana kama kimevuka mipaka ya nchi,kitanangwa na kupewa kila sifa mbaya ndani ya jamiiforums kupitia wafuasi wa chadema .akitokea mwandishi wa habari hasa wa tv akimsifia rais wake wan chi au prof lipumba kwenye luninga hapo ataona chamte makuni, ataanikwa na kuanuliwa kisa kwanini amsifie .
Viongozi wakuu wa chadema ambao wanashiriki mijadala wamekuwa kimya , huku media hiyo ikionekana mbele ya sura za watu kama media ya Chadema, huku wao wakiwa mbele kutetea uhuru wa kutoa maoni sehemu nyengine, hiyo ndio chadema inayopigania kuongoza Tanzania yenye amani na utulivu .ukihoji upi msimamo wa chadema kuhusu mahakama ya kadhi na Oic wakati vyama vyengine misimamo yao ipo wazi hapo utapachikwa jina baya pengine kuitwa alqaida ndani ya jamiiforums, ukihoji Elimu ya Dk slaa itasaidiane jamii ya kitanzania hapo utasakamwa na utaichukia jamiiforums, lakini kweli leo kama watanzania pangalitokea mgombea mwenye elimu ya “master in Isalmic law” watanzania wangaliogopa kuhoji?kwanini tuogope?
Imefika wakati viongozi wa chadema kwamba wasiamini jamiiforums ndio kipimo cha ushindi, ndio maoni ya watanzania, wajue wachangiaji ambao sio wapenzi wa chadema huona michango inayotolewa na wanachadema ukumbini ndio mawazo ya chama, kejeli zinazotolewa na wanachadema ndio mawazo ya makao makuu lakini kufungia watu huku wenyewe wachangiaji na invisible huku mwenyewe wakipigania uhuru upande wa mbili hii inaweza kuweka sura mbaya kwa chadema na kwa jamiiforus kwa ujumla ,lakini hii pia inawavunja moyo wachangiaji ambao wanamawazo mazuri na nchi yetu hii, kwani chadema kama chama kinachoongozwa na binaadamu kinahaitaji kukosolewa ili kijijiue na kijipange. Chadema imeingia kwenye uchaguzi mengi yatasemwa kupitia vyombo vya habari, vipo vitaunga mkono 100% lakini vyengine vitakuwa kinyume na wao kwa 100%, yote hayo wavivumilie kama anavyovumilia JK, hawa ndio watanzania wenye mawazo tofauti, kama chama kinatakiwa kisimame imara kujitetea kuhusu udini ndani ya chama baada ya taarifa ya upadri wa dk slaa kutolewa kwani taarifa hizi bado zinaripotiwa kwenye vyombo vya habari ambavyo vinaingia hadi vijijini tofauti na jamii forums ambayo inasomwa na watu wachache tena ni wasomi tu ,lakini pia jamiiforums inaonekana dunia nzima kwa hivyo inawezekana baadhi ya wanaojadili sio wapiga kura na wanaishi mbali na Tanzania , kama chadema haitojibu hoja hizi kwa umakini mkubwa bila ya vitisho chama kinaweza kukosa wafuasi mikoa yenye waumini tofauti na imani ya Mgombea na kunyima kabisa matarjio ya chadema kuongoza nchi na kuipa ushindi wa kishindo ccm.

Mungu amjaalie Jk ashinde kwa kishindo, 88% inatosha
Malariasugu@yahoo.com
www.jktu2010.blogspot.com

No comments:

Post a Comment